GET /api/v0.1/hansard/entries/1557577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1557577,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557577/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nami niunge mkono mjadala wa leo kuhusu uteuzi wa Mhe. Susan Nakhumicha. Ninajua mambo mengi yametokea. Lakini, anastahili. Hasa ukiangalia ukakamavu wake wa kazi na masomo yake. Ndio, yalitokea ya kutokea katika Wizara ya Afya. Sio mwaka wa kwanza yakitokea akiwa hapo. Yametokea wengine wakiwa hapo, kama madaktari kugoma. Kwa hivyo, ni taifa liangalie mishahara na mambo ya madaktari, walimu na wengineo. Nakhumicha ni mama na alionyesha. Mimi kama mama siwezi kumvuta mama mwenzangu chini kwa sababu najua aliweza na anaweza. Hata kama pengine ametoka nafasi kubwa na kurudi ya chini, lakini pia anaweza kuserve taifa lake akiwa pale. Kwa hivyo, ninaunga uteuzi wake mkono. Ninamuombea Mungu afanye kazi yake akiangalia maslahi ya Wakenya na kuyaweka mbele."
}