GET /api/v0.1/hansard/entries/1558419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1558419,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558419/?format=api",
    "text_counter": 240,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Edwin Sifuna kwa huu Mswada wake. Huu ni Mswada wa maana sana kwa vijana wetu ambao wanariadha mara nyingi katika nyanja ya michezo. Kwa mfano, wakimbiaji kutoka Kaunti ya Nandi, ambako Sen. Cherarkey anatoka, na pia ni mashemeji wangu, wachezaji mpira kutoka kaunti mbalimbali, na wanaocheza michezo inayojulikana kwa kizungu kama indoor games. Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema wazi kwamba kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa wachezaji wetu kufanya michezo kwa sababu ya ufadhili. Timu nyingi za soka ambazo zinacheza nyanjani sehemu za mashinani sana, Wazungu huita rural areas, zina changamoto ya fedha sio haba. Timu inayofaa kusafiri The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}