GET /api/v0.1/hansard/entries/1558430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1558430,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558430/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninajua asili mia moja hii ni nyingi kwenu. Ninafahamu mnafaa kutoa huduma mbalimbali kama vile afya, maji na kilimo bora. Vile vile, vijana wetu wanahitaji usaidizi na ufadhili. Zile pesa zikikufikia pale kwa Wizara ya Michezo katika kaunti zetu, ninaomba magavana, mawaziri wa fedha na wale wa michezo wawe wepesi kuhakikisha fedha zile zimefikishwa kwa makundi ya vijana pasipo na utepetevu wowote wala kucheleweshwa ili tuone matunda yake."
}