GET /api/v0.1/hansard/entries/1558972/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1558972,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558972/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Mhe. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "hawana uwezo. Hapa nina sisitiza neno uwezo. Katika mkataba wa uwezo, tunazungumzia mafukara. Fukara ni mtu ambaye hana chochote. Hajui atakula nini na atalala wapi. Maskini ni mtu ambaye anacho lakini alicho nacho hakimtoshi. Kwa mfano, maskini angetaka kula chapati mbili lakini hana uwezo hivyo basi inamlazimu ale chapati moja au nusu pamoja na familia yake. Mswada huu unafuata mfumo wa dini kuwa kama jamii, ni lazima tuwasimamie wasiokuwa navyo. Fedha ambazo wahitaji watapewa ni ushuru ambao unatozwa wafanyakazi na wafanyabiashara wanaopata faida. Kwa hivyo, ni mfumo mzuri ambao utahakikisha wahitaji wanasaidika. Sioni kama mwaka ni kigezo kizuri kutumika kwa sababu kuna uwezekano wa mtu kuwa na miaka zaidi ya 60 kama inavyosema sheria lakini ana uwezo. Katika mfumo wa NG-CDF ambao unafaa iwe ya kumfaidi mlala hoi asiyekuwa na uwezo, wale wenye uwezo hujaza form zetu na kusema kuwa hizo fedha ni za Serikali na ni za bure. Ninahofia kuwa ikiwa miaka ndio kigezo watakachotumia peke yake kutakuwa na uwezekano wa mtu aliyefikisha miaka 60 kusema anastahili kupata usaidizi huu ilihali ana uwezo. Hilo litasababisha upungufu wa fedha zitakazotolewa. Nataka kuongezea kuwa fedha hizi zisitolewe kwa usawa. Kwa mfano, ikiwa ni elfu mbili au tatu eti kila mhitaji apate hizo elfu mbili au tatu. Tunavyojua, watu wana mahitaji mbali mbali. Bodi ikiundwa, itengeneza kanuni zitakazotumika kubaini hali halisi ya watu ili anayestahili elfu tatu apewe hizo elfu tatu kulingana na uwezo wa familia yake na anayestahili elfu kumi apewe hizo elfu kumi kwa sababu ya majukumu au maradhi aliyo nayo. Watu wapewe fedha kulingana na mahitaji yao. Kusiwe na kiwango maalum cha fedha zitakazopewa wahitaji kwa kuwa mahitaji ya watu si sawa. Ahsante."
}