GET /api/v0.1/hansard/entries/1558986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1558986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558986/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie Mswada huu. Huu Mswada umenifurahisha na utawafurahisha wale ambao wametuchagua. Mswada huu umeletwa bungeni kwa sababu Serikali inataka kuweka mikakati ya kuwasaidia watu walio na shida katika hii nchi yetu ya Kenya. Watakaofaidika ni wale wasiojiweza katika jamii wakiwemo wazeee, wajane na mayatima. Huu Mswada utaleta raha kwa watu ambao hawajiwezi katika jamii yetu. Huu ni Mswada wa maana sana. Mswada huu utatoa nafasi kwa Serikali kupeleka mafunzo hadi mashinani ndio ijulikane ni nani ana shida ndio Serikali itengeneze mikakati ya kujua ni nani atafaidika na mambo kama haya. Wakati wa uongozi wa His Excellency, the late President Moi, watoto walikuwa wakinywa maziwa ya Nyayo."
}