GET /api/v0.1/hansard/entries/1558994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1558994,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558994/?format=api",
    "text_counter": 234,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Asante. Yale yote niliyosema yameeleweka na watu wangu. Pengine watu wake hawawezi kuelewa Kiswahili changu. Lakini nimechagua kuzungumza kwa Kiswahili kwa sababu ninataka watu walionichagua kuelewa ninachosema katika Bunge hili. Na watu wangu wanaelewa. Kwa hivyo, kuhusu Mhe. Ruweida, yeye ataendeleza masomo kule kwao. Samahani, amenipotezea muda. Huu ni Mswada unaoanzisha mkakati wa kuwasaidia wale wanaohitaji msaada. Wataweza pia kupata taarifa kuhusu mpango wa Serikali. Kwa hivyo, wanaponisikiliza hivi sasa, wanajua kuwa kama wao ni wajane, pia watapata usaidizi kutoka kwa Serikali yetu. Kitu cha maana ni mkakati unaoandaliwa na Serikali kwa ajili ya wananchi wake. Sisi ni tofauti katika nchi yetu ya Kenya. Wale tunaowazungumzia ni wazee wasio na usaidizi wowote; hata hawana makazi. Mambo tunayojadili katika Bunge hili yamewekwa ndani ya Katiba ya Kenya. Kwa hivyo, Mswada uliowasilishwa hapa umetayarishwa ili kutoa mkakati mzuri wa kuwanufaisha wananchi wa Kenya. Mimi, kama Mwakilishi wa Nakuru, nimewasikiliza. Ninaunga mkono kwa asilimia mia moja."
}