GET /api/v0.1/hansard/entries/1559193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1559193,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1559193/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, WDM",
"speaker_title": "Hon. John Bwire",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika. Kifungu cha 56 cha Katiba ya Kenya kinatoa mwelekeo kwamba Serikali itafanya mipango ya kutambua jamii ndogo nchini Kenya. Hiyo mipango itaongeza mambo ya utawala, kazi na kutambua mila na desturi zao. Ninakumbuka ulipokuja Eneo Bunge langu mwaka wa 2023, wazee walio mbele yako leo walikueleza kwamba wangetamani sana watambulike kama moja ya makabila ya Kenya. Ninakumbuka hiyo siku uliwaeleza kwamba kuchelewa kutambulishwa kwao ni kinyume cha Katiba. Na kwamba, kama jamii zingine kama vile jamii ya Wasomali kwenye mpaka wa Kenya na Somalia, Waluo katika mpaka wa Kenya na Tanzania, na Wakuria katika mpaka wa Kenya na Tanzania, Wapare walioko kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania kule Taveta, watambulike. Leo hii, ninatoa shukrani kwa niaba ya kamati ya wazee wa Wapare wanaoishi sehemu zingine za Kenya na Eneo Bunge la Taveta. Ninakushukuru Mhe. Spika na Bunge hili la Kitaifa kwa kuwapatia nafasi ya kuleta malalamishi yao Bungeni. Wamesikilizwa na wamepewa hakikisho kwamba maombi yao yataangaliwa. Ningependa kusema jambo moja tu kabla niketi. Mwaka wa 2022, mmoja wa jamii hii, alipendekezwa kuwa mwakilishi kata maalum kwa Chama cha Wiper ilhali nafasi ilichukuliwa. Baada ya kuenda kortini, korti ikasema kuwa kwa sababu Wapare wanatambulika kama wasio na nchi, waliwekwa kimakosa katika orodha ya jamii walio wachache nchini ilhali hali sio vile. Kwa hivyo, hatua hii ambayo imechukuliwa na Bunge la kitaifa leo ni ya kipekee sana. Ninachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Spika na Wajumbe wenzangu kwa kuwapatia Wapare nafasi hata ya kufika Bunge leo. Wengine wao wameniambia hawajawahi kutambulika katika Bunge la Kitaifa. Mhe. Spika, asante kwa kuwatambua leo na Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki. Asante Sana."
}