GET /api/v0.1/hansard/entries/1559196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1559196,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1559196/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Pia nami, ninawapongeza wazee Wapare waliopata nafasi ya kufika Bunge hili. Pia, natilia mkazo na nguvu kwamba watambuliwe. Kule mashinani, wanapata shida kubwa kuanzia hao wazee mpaka watoto wao. Hata katika shule ya msingi siku hizi, lazima uwe na stakabadhi ya kuzaliwa ndio usajiliwe kama mwanafunzi. Inakuwa ni vigumu kwa watoto na wajukuu wao. Hii ni jamii ya Kenya. Hawaishi mahali pengine. Wanaweza kuwa upande wa Tanzania, lakini Wapare wengine ni Wakenya, ambao tuko nao mpaka Eneo Bunge ya Kisauni na sehemu zingine. Kwa hivyo, nasimama hapa kutilia nguvu watambuliwe kama Wakenya kwa haraka kama jamii ya Pemba. Wale waliobaki waendelee kutambuliwa, bora wako Kenya, ili kusudi waweze kuajiriwa na kufanya mambo yote raia wanafanya. Mhe. Spika, nimesimama kuunga mkono na kusisitiza hili jambo lichukuliwe kwa haraka, ili wasipate tabu na adhabu wanazoendelea kupata."
}