GET /api/v0.1/hansard/entries/1560002/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560002,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560002/?format=api",
"text_counter": 993,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "hutia sahihi. Kwa hivyo, ni muhimu sana sheria hizo kutambulika kinaga ubaga haswa na Bunge la Kitaifa. Ili mikataba hii ikubalike, ni mujibu wa Bunge kutengeneza sheria nchini ambazo pia zinaambatana na Katiba yetu. Hivyo, nchi yetu inatambulika ulimwengu mzima kukubaliana. Mhe. Murugara amezungumzia kwa uwazi vifungu ambavyo vinahusiana na Mswada huu. Vifungu hivi vimeguzia maswala muhimu sana. Kwa sababu, ni lazima tujue faida na madhara ya mikataba hii katika taifa letu. Mfano ni sheria za mikataba ya kibiashara kama zile zinazohusiana na maswala ya ushuru. Je, tukikubaliana na mikataba hii, tutaboresha au kudidimiza uchumi wetu? Vile vile, mikataba hii huwa na mambo ya kisiasa yanayopinzana na tamaduni zetu. Mikataba mingi huzungumzia haki za kibinadamu. Hivi majuzi, tumeona nchi kadhaa zimekubaliana na ndoa za kijinsia. Je, iwapo mkataba kama huu hautaletwa Bungeni na sisi kufanya mashauriano, basi unaweza kutuleta madhara katika mila na tamaduni zetu za kidini za Kiisilamu na Kikristo. Kwa hivyo, suala kama hili ni suala muhimu sana. Pili, wakati wa kuadhimisha siku ya kina mama, huwa tunaenda mkutano mkubwa kule Amerika ili kuzungumzia haki za kimsingi, haswa haki ambazo zinaangalia masuala ya akina mama, watoto na walemavu. Siyo Wabunge wote wanaenda pale. Ni wachache ambao wanachaguliwa kuhudhuria mkutano ule. Wakati mwingi, unapata nchi yetu inaweka sahihi bila kuangalia mkataba vizuri. Halafu, baadaye tunaona unakiuka mila na desturi zetu ama Katiba ya taifa letu la Kenya. Mswada huu pia umezungumzia kwamba utatengeneza wakala ama gazeti ambalo litatangaza mkataba wa sheria ya kiulimwengu kuhusu jambo fulani. Kwa hivyo, Wakenya wataweza kuelewa na kufahamu. Kama Katiba inavyosema, Wakenya wapate uhuru na nafasi ya ufahamu ama kuelezwa mambo yanajiri na kupata mawasiliano ya mambo ambayo yanayotukabili katika taifa letu la Kenya. Kwa hivyo, gazeti hilo likitolewa wakati unaofaa, Wakenya watalipitia na kuwafahamisha Wabunge wao kuwa mkataba huo una madhara ama faida gani, na iwapo wanaukubali au la. Hili ni jambo la maana sana. Vile vile, Wabunge wataweza kushauriana na Waziri mhusika kama mkataba wa kimataifa unalingana na sheria na sera zetu, kabla haujaidhinishwa kikamilifu na kuchapishwa. Hivi sasa, nafikiri suala hili haliko. Tukipitisha Mswada huu na kutiwa sahihi na Rais wetu, ambaye tunamheshimu sana, utapatia nafasi Waziri na Wabunge kushirikiana na kufanya mazungumzo ili kupata mwongozo kuhusu iwapo tufuate sheria hiyo na kuithibitisha au tukatae kuithibitisha. Vile vile, tutaweza kupata nafasi muafaka ya kupiga msasa. Hii mikataba huwa kama sheria ambazo tunatengeneza katika hili Bunge la Kitaifa. Mikataba hiyo ina vifungu na maneno mengi sana kama sheria nyingine. Tutaangalia iwapo, baada ya kuikubali mikataba hiyo, tuna uwezo wa kuunda sheria katika Bunge letu ili uthibitisho uwe sawia. Hii itahakikisha kuwa tupo pamoja na yale mataifa yaliyokubaliana na mikataba hiyo. Mara nyingi, sheria hizi huwa zinakuja kisiasa sana. Unapata nchi ambazo zimejiweka pamoja, zina ushirikiano fulani wa kisiasa ama wa kibiashara na wanakubali mkataba huo. Unapata kuna nchi zingine ambazo hazishirikiani na baadhi ya mataifa katika masuala ya kisiasa ama wana mizozo au tofauti za kibiashara na, kwa hivyo, hawaungi mkono. Wakati mwingine mnajipata mumeingizwa katika mkataba na kumbe wale ambao wamekubaliana na mkataba ule ni mahasimu wa marafiki wenu katika nchi kadhaa."
}