GET /api/v0.1/hansard/entries/156011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 156011,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/156011/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasiya kuchangia Hoja hii. Kwanza nataka kutoa shukrani nyingi sana kwa Kamati iliyofanya kazi kwa haki na usawa na ambayo ilizingatia maadili ya taifa. Walichagua watu bila kuzingatia misingi ya kikabila. Ningependa kusema kwamba uongozi wa nchi hii ni lazima utambuliwe. Mtu yeyote anayetumikia taifa hili kwa mapenzi na moyo wake wote inafaa atambuliwe. Shida tuliyo nayo na iliyoweka nchi hii katika matatizo makubwa ni kwamba hatuna shukrani kwa utumishi wa nchi. Mtu yeyote aliyetumikia taifa hili kutoka mwanzo mpaka leo, mchango wake hauonekani kama mchango wa taifa, bali unaonekana kama mchango wa kikabila."
}