GET /api/v0.1/hansard/entries/156013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 156013,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/156013/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tukiangalia katika nchi nzima, watu wengine wanasema kwamba unapozungumza juu ya uongozi wa taifa hili basi usimuweke Mkikuyu ndani kwa sababu Wakikuyu walitoa Kenyatta na Kibaki kama rais. Hivi inamaanisha kwamba ni wakati wa wengine kuingia vile vile na kula. Mimi ningependa kusema kwamba uongozi wa nchi sio uongozi wa kikabila. Wakati Kenyatta alichukua uongozi, hakuchukua kwa mabavu bali alichaguliwa na wananchi vile tumeweka hawa katika mamlaka ili watutumikie. Bw. Kibaki alipoingia, hakupitia mlango wa nyuma bali alipewa kura na wananchi kama Mkenya ili kuongoza taifa hili. Hayo ndiyo maadili ambayo tungependa kuzingatia ili tumalize ukabila kabisa."
}