GET /api/v0.1/hansard/entries/156014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 156014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/156014/?format=api",
"text_counter": 327,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Kamati hii ilipoketi chini, ilifanya kazi nzuri. Waliweka wanawake tisa kati ya wanachama 15. Wanawake ndio wanaoyaona matatizo na mateso ya nchi. Wanawake ndio wanaokimbia na watoto na wanajua hata shida ya kuzaa na pia wanaelewa shida za wananchi kwa jumla. Kwa kumalizia, ningependa kusema kwamba, tunapoanza masuala ya kuongoza nchi, tunataka tuweze kuweka utumishi wetu katika mashinani na tuwe watu wa kusema ukweli. Mambo yamesemwa hapa hata yale ya mahindi. Mahindi ni jambo ambalo limezungumziwa na linaendelea na bado linazua taharuki kubwa hata katika bunge hili. Mimi ninaona kwamba swala hili litaendelea kuwa ngumu. Nataka kuwaomba wenzangu kwamba tunapolitaja jambo hili wasiseme kwamba âwanamaliza kabila letu.â Ningependa tujitoe mhanga na tupandishe ngazi yetu kwenda juu katika uongozi na mambo ya ukabila au kusema kwamba huyu ni ndugu yangu, tusahau kabisa. Kwa kweli, haingefaa kununua mahindi kutoka Africa Kusini kwa Kshs2,600 kwa gunia moja ya kilo 90. Wangenunua hapa katika nchi yetu kwa Kshs2,500 ili wakulima wetu wapate hela ya kujisaidia na kulipa madeni yao katika benki na kulipa karo ya watoto wao. Vile vile, wanabiashara wangepata pesa. Tunavyoona gharama ya kuleta hayo mahindi katika nchi hii ilikuwa ni Kshs1,200. Kwa hivyo, jumla ya gharama ni Kshs3, 800. Hayo mahindi yalipofika Mombasa, subsidy ilikuwa ya Kshs1,750. Yanapouzwa hayo mahindi, yanauzwa kwa Kshs2,000. Hii inamaanisha kwamba Serikali inapoteza Kshs1,950. Sitaki kuzungumzia maneno ya mtu wala sitauliza ama kwamba yeye ni mkabila. Lile jambo ninaweza kusema ni kwamba nchi imepoteza pesa kiasi ya Kshs4 billioni. Tunapozungumza, utasikia wengine wakisema kwamba hii ni siasa. Walioko uongozini, waongoze bila ya kutumia lugha isiofaa."
}