GET /api/v0.1/hansard/entries/1560352/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560352,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560352/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Sijui suala hili la ardhi na wananchi kunyanyaswa tuliimbie, tulizungumzie au tulililie ili wananchi wapate haki yao. Sio tu watu wa Kuria peke yake walioathirika. Kila wakati tunalizungumzia hili suala la ardhi, haswa sehemu za Pwani kama Matuga na Kwale ambako watu wananyanyaswa kila kuchao... Kuna sehemu kama Darad kule Diani, ambako watu wenye vibali walivyopewa na Serikali bado wananyanyaswa na mabwanyenye. Naunga mkono ardhilhali hii iliyoletwa na Mhe. Marwa Kitayama kwa niaba ya watu wake wa Kuria. Kama walivyozungumza wenzangu, itafika wakati ambapo kwa sababu ya suala hili, tutalazimika kuwa na vikao maalum, kama Wabunge, kuona ni vipi tutabatilisha sheria za tume ya mashamba, the National Land Commision Act, ili iwe na nguvu; na vipi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}