GET /api/v0.1/hansard/entries/1560935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560935/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Msambweni, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Feisal Bader",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya 44(2)(c), naomba Kauli kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kuhusu unyakuzi wa ardhi ya umma ya Msikiti wa Kongo katika Eneobunge la Msambweni. Mheshimiwa Spika, Msikiti wa Kongo una dhima ya kihistoria na kidini, kwa kuwa ulijengwa katika Karne ya 14 na Waajemi (Persians). Msikiti huu ulitambuliwa kwa mara ya kwanza kama kumbukumbu la kitaifa na Serikali ya mkoloni mnamo mwezi Juni mwaka wa 1927. Baada ya Kenya kupata uhuru, Msikiti wa Kongo, pamoja na ardhi inayouzunguka, ulitangazwa rasmi kuwa kumbukumbu la kitaifa lililolindwa chini ya sheria. Hata hivyo, mnamo mwaka wa 1986, inadaiwa kwamba watu fulani walishirikiana na maafisa waandamizi wa Serikali kutekeleza njama ya kumilikishwa ardhi hiyo kwa Rais wa wakati huo, hayati Daniel Toroitich Arap Moi, kwa njia ya udanganyifu na isiyo halali. Mnamo mwaka wa 2009, akiwa amestaafu, hayati Rais Moi alifahamishwa kuhusu umilikishaji huo usiyo halali na kwa hiari yake, alirejesha hati miliki ya ardhi hiyo kwa msajili wa hati. Hatua hii ilipelekea kubatilishwa kwa hati miliki hiyo na kurejesha hali ya umiliki wa ardhi hiyo kuwa ya umma, kama ilivyotambuliwa tangu mwaka wa 1927. Mhe. Spika wa Muda, kutokana na hatua hizo, Serikali ilitenga ardhi hiyo kwa manufaa ya jamii ya Waislamu wanaoswali katika Msikiti wa Kongo na kutoa hati mbili: Hati Nambari 55034 kwa Msikiti wa Kongo na Hati Nambari 55035 kwa Kituo cha Kiislamu cha Kwale. Serikali iliteua Katibu Mtendaji katika Wizara ya Hazina ya Taifa kuwa mdhamini wa hati miliki ya ardhi hiyo. Mnamo mwaka wa 2012, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Mhe. Raila Odinga, maarufu Baba, alizikabidhi hati miliki hizo kwa jamii-nufaika. Mnamo mwezi wa Machi 2025, jamii hiyo ilishangaa kugundua kuwa kipande hicho cha ardhi kilikuwa kimetangazwa kuuzwa kwa bei ya shilingi bilioni moja, milioni mia nne arobaini na tano (Ksh1.445 bilioni). Watu wanaodai kumiliki ardhi hiyo ni Bwana Mohammed Hamisi Mwachumba na Bwana Ali Mwadarashi Mwagariche. Wanadai kuwa walipata hati miliki ya ardhi hiyo tarehe 17 Februari 2025. Jambo ambalo linastaajabisha ni kuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}