GET /api/v0.1/hansard/entries/1560936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560936,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560936/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Msambweni, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Feisal Bader",
"speaker": null,
"content": "inafahamika kwamba ardhi hiyo imekuwa ya umma tangu mwaka wa 1927 na kudumishwa baada ya Kenya kuwa nchi huru. Mhe. Spika wa Muda, ni kutokana na hali hii ndipo ninaomba kauli kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kiidara ya Ardhi kuhusu masuala yafuatayo: 1. Maelezo kuhusu namna ambavyo ardhi ya Msikiti wa Kongo, inayojulikana kuwa ardhi ya umma na iliyotangazwa kama eneo la kumbukumbu la kitaifa lililolindwa, ilisajiliwa kwa umiliki wa kibinafsi. 2. Hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Ardhi pamoja na Tume ya Kitaifa ya Ardhi kukabiliana na unyakuzi huu wa ardhi ya Msikiti wa Kongo. 3. Mikakati iliyowekwa kulinda eneo hilo kama kumbukumbu la kitaifa linalolindwa. 4. Maelezo ya kina kuhusu jinsi Wizara pamoja na Tume ya Kitaifa ya Ardhi zinavyokusudia kuwezesha kurejeshwa kwa ardhi hiyo kwa wamiliki halali ambao ni jamii ya Waislamu wa Msikiti wa Kongo. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}