GET /api/v0.1/hansard/entries/1560938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560938,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560938/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nataka ibaki katika kumbukumbu za Bunge hili kwamba naunga mkono Kauli iliyoletwa na Mbunge wa Msambweni. Yeye ametoka katika eneo bunge ambayo mimi pia ninamiliki. Sisi, kama watu wa Kwale, tulitamaushwa pakubwa na jambo hili. Mimi naunga mkono Kauli hii. Hii ni kwa sababu mimi ni mtoto wa Kiislamu na ninaelewa historia kamili kama vile Mhe. Feisal alivyo izungumzia. Ardhi ya Msikiti wa Kongo ni pahali patakatifu. Ni jambo la kushangaza vile wezi na walaghai walikuja na kusema ardhi ile wao ndio wamiliki. Historia inajieleza vizuri sana kwamba ardhi ile ni ya msikiti. Ilipatikana kwa njia gani? Mhe. Feisal ameeleza historia. Haiwezekani kuwa mtu ametokezea hivi majuzi na anasema anataka kumiliki ardhi ile ya kihistoria. Ardhi ya Kongo haiuziki na haiwezi kuuzwa. Nina laani vikali jambo hili. Pia, naongezea Kamati ya Kiidara ya Ardhi ya Bunge hili iweze kuingilia kati. Hii ni kwa sababu historia inajieleza vizuri sana. Wacha nikome hapo. Asante sana."
}