GET /api/v0.1/hansard/entries/1560966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560966,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560966/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, ODM",
"speaker_title": "Hon. Irene Mayaka",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuchangia kauli ya Mheshimiwa ambayo inazungumzia swala la ardhi za kihistoria. Ardhi za kishitoria na za kidini ni mambo ambayo Kamati inayohusika inafaa iangalie kabisa. Inafaa tuwe na sera ili kama taifa tujue ni wapi ambapo tuko na ardhi za kihistoria ambazo hazijateuliwa, hazijalindwa au kuzingatiwa katika sheria. Ili tuhakikishe zimekuwa na ulinzi ambao uko murwa kabisa. Ninamshukuru Mheshimiwa kwa kuleta kauli hii. Kamati ambayo itaenda kuangalia jambo hili iangazie ni sera gani tunaweza leta ili swala la ardhi za kihistoria litatuliwe kisawa. Asante sana."
}