GET /api/v0.1/hansard/entries/1560968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1560968,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1560968/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sotik, UDA",
"speaker_title": "Hon. Francis Sigei",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kuunga mkono kauli hii ambayo imeletwa na Mhe. Feisal. Mambo ya ardhi katika nchi hii yamekuwa chanzo cha maafa na watu kunyakua ardhi ya wengine au jamii. Niliuliza Mhe. Feisal ni kiasi gani cha hilo shamba kimenyakuliwa. Aliniambia kuwa ni ekari 16. Hili ni jambo ambalo linazidi Kamati inayohusika. Ninapendekeza kwamba Waziri wa Ardhi aweze kufika hapa baada ya likizo tunayoelekea leo. Hili ni jambo ngumu sana kwa maana kuna watu wamenyakua shamba hata za shule. Ni lazima Serikali ishughulikie jambo hili kwa njia inayotakikana. Ninapendekeza kuwa Waziri wa Ardhi aweze kufika hapa ili atueleze mambo mengi yanayohusu ardhi. Asante sana."
}