GET /api/v0.1/hansard/entries/1561314/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1561314,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561314/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika. Kama mama Mombasa, leo nimetamaushwa sana. Watu wetu wameweza kuomba ufadhili wa pesa za National Gender and Affirmative Action Fund (NGAAF). Ni vikundi ambavyo Rais wa taifa alisema anataka kuinua kiuchumi. Rais akatuongozea pesa sisi kina mama ili ziweze kusambaa mashinani. La kusikitisha ni kuwa wanawake, hasa kina mama 47 katika Bunge hili, wamedharauliwa sana. Juzi hapa nilimuuliza Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi hizi pesa zilikatwa vipi?. Akasema zilikatwa hapa Bungeni. Tukija kuangalia, hazikukatwa hapa; zilikatwa kule Treasury . Nataka niwaeleze Wakenya hawa, kina mama 47 munaowana leo Bungeni, wakija kule mashinani, nawomba muwaelewe kuwa pesa zao zimekatwa. Kama kuna vikundi vilikuwa vimeomba ufadhili wa NGAAF, nawaomba mujue kwamba makundi mengi yatakosa pesa. Msiwapige hawa kina mama kule mashinani."
}