GET /api/v0.1/hansard/entries/1561315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1561315,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561315/?format=api",
    "text_counter": 103,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hayo yote Mhe. Spika, namuomba Waziri Wa Fedha na Mipango ya Uchumi aturudishie Kshs500 milioni alizokata. Namuomba Waziri atoe maelezo kwa sababu nimeona tangazo kwenye gazeti kuhusu mambo ya sanitary towels . Sisi ni kina mama 47, lakini kwenye tangazo hilo, wameorodhesha kaunti 17 pekee. Kule kwetu Mombasa haijaonekana. Watasema mama Zamzam amekula pesa. Leo huyu wa Busia ataambiwa amekula pesa. Kaunti ni kubwa na pesa yetu ni kidogo. Badala tuongezewe, tunafinywa. Rais alisema atawatetea kina mama. Rais leo nakuomba kwa unyenyekevu, kwa sababu una nguvu na uwezo. Muite Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi aje aturejeshee pesa zetu, tuingie mashinani tufanye kazi ili kazi yako ionekane."
}