GET /api/v0.1/hansard/entries/1561441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1561441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561441/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
    "speaker": null,
    "content": "Juzi tu mwezi wa Novemba, Mhe. Sunkuli aliomba kauli kwa ajili ya mambo haya haya na wakati huo, alizungumzia maeneo ya Angata Barrikoi, Guitembe na Mpakani ambapo jirani zetu Wakuria na Wakipsigis wanazozana. Wakati huo, ilionekana kuwa ni jambo lililohitajika kuzingatiwa kwa dharura. Nakushukuru, Mhe. Spika, kwa sababu ulitoa agizo kuwa Kamati ya Utawala na Usalama wa Ndani inayoongozwa na rafiki, ndugu na jirani yangu, Mhe. Tongoyo, iende katika eneo la tukio hilo kuangalia ni nini tunachoweza kufanya ili usalama upatikane. Mhe. Spika, ulinituma kikazi kule Dubai, lakini nilikatiza safari yangu kwa siku mbili mfululizo na kurudisha hela ulizokuwa umenipatia kusafiria kwa sababu hili ni jambo nyeti. Tulienda katika eneo la tukio na tukajaribu kuangalia mahali shida ilikuwepo. Naishukuru sana Kamati kwa sababu walisikiliza watu wetu na wakapata uhalisia wa mambo. Bunge hili linajua kuwa shida katika eneo hilo ilianza tangu miaka kabla ya Kenya kupata Uhuru. Ukweli ni kuwa tumekataa kufuata haki kama nchi. Tunafanya hivyo makusudi tu. Namuunga mkono jirani yangu, Mhe. Sunkuli. Nasikitika sana na kutoa rambirambi zangu kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao na mali yao. Matatizo yanaendelea katika ukanda ule. Nilipoanza, nilisema kuwa mla huliwa. Damu ya binadamu ni damu ya binadamu. Haitoi picha na taswira nzuri kuwa wiki mbili au tatu zilizopita, Wakuria waliuwawa katika eneo hilo lakini sikuona hali ya dharura ninayoona sasa hivi. Maafa tunayojutia sasa hivi yanaonekana kama ni makubwa zaidi kuliko yale yaliyofanyika kwa jamii ya Wakuria. Ukanda huu hauhitaji mjadala wa kupapasa papasa, bali unahitaji mjadala halisia. Kila mtu anayezungumzia mambo ya eneo hili anazungumzia historia. Sisi kama Wakuria tuna historia yetu. Wakipsigis wana historia hiyo. Ndugu zetu wa jamii ya Maa ni jirani zetu wazuri sana, na wana historia yao. Tunakubaliana kuwa jamii zote zilizoko pale za Maa, Sirikwa, Moitanik, Wakuria, Wakisii na wale wote waliomiliki mashamba pale, tuishi kwa sawa na kwa haki kwa sababu Katiba yetu inatupatia haki. Haipendezi kuwa Kamati hii..."
}