GET /api/v0.1/hansard/entries/1561788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1561788,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561788/?format=api",
"text_counter": 576,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
"speaker": null,
"content": "Mara nyingi huwa najiuliza, kama sekta ya bodaboda haingekuwa, vijana wetu wengi wanaotoka shule saa hizi, wangekuwa wanafanya kazi gani? Ninavyojua, hali ya uchumi katika nchi yetu si nzuri vile. Vijana wengi wamepata makao katika sekta hii ya bodaboda. Wanajipatia riziki ya kila siku ili kuweza kujiendeleza katika maisha yao. Kwa hivyo, sekta hii imechangia pakubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Ganze ni sehemu ya mashambani, yaani rural area . Hakuna barabara. Nafikiri katika Eneobunge lote la Ganze, kilomita za barabara zilizowekwa lami hazifiki hata thelathini. Sisi kama wakaazi wa Ganze tunategemea sana usafiri wa bodaboda kufanya biashara zetu na pia kutoka mahali moja hadi nyingine. Ingekuwa hamna pikipiki, watu wangekuwa wanasafiri kwa miguu au kupitia baiskeli. Mara nyingi, inakuwa vigumu sana kusafirisha bidhaa ama watu, sana sana wagonjwa. Lakini sasa hivi, ukipatikana na shida katika nyumba yako hata kama ni usiku wa manane, ni rahisi kumuita mtu wa bodaboda aje akupeleke hospitalini. Hospitali kule Ganze pia ziko mbali sana. Kila hospitali ni zaidi ya kilomita kumi kutoka kule wananchi wanakoishi na kwa hivyo, kuwafikia kwa urahisi huwa shida. Lakini kwa sababu ya uwepo wa bodaboda, sisi kama wakaazi wa Ganze, tumeweza kupata huduma tofauti kwa urahisi. Sekta hii iko na manufaa mengi sana. Tukianza kuyataja moja baada ya nyingine, pengine tutakesha hapa tukizungumzia mambo haya. Lakini kila kizuri pia hakikosi ubaya wake. Kuna watu wachache ambao wanaharibu jina nzuri la uhudumu wa bodaboda. Kuna wengi ambao wamejipanga vizuri, wamekuwa katika sekta hii kwa muda mrefu na wamejiendeleza. Wameendesha maisha yao vizuri na wametengeneza Sacco yao . Ijapokuwa walianzia kwa kuandikwa kama waendeshaji wa bodaboda, kwa sababu ya uadilifu wao, wameweza kununua bodaboda zao binafsi. Hao ni wale wamejipanga. Lakini kuna wachache wanaoharibu jina la sekta hii kwa kuingiza uhuni na kufanya mambo yasiyostahili. Wahalifu wengi wanaohusika katika uporaji wa mali ya watu na majangili wanaohusika na visa vya mauaji, hutumia bodaboda wakati mwingi kutekeleza uhalifu huo. Wengi wanaofanya kazi ya bodaboda wanafanya kazi nzuri sana na wanastahili kuungwa mkono. Kama nchi, ni muhimu tutunge sheria ambazo waendeshaji wa bodaboda watafuata. Sisi kama watumizi wa barabara, huwa tunawaona waendeshaji wa bodaboda wakivunja sheria za barabara. Unajipata unaendesha gari lako katika ule mkono wako wa kulia wa barabara lakini mtu wa bodaboda anaupitia mkono huo huo bila kujali kuwa anaweza kusababisha ajali. Tumeona mara nyingi sana katika barabara zetu ajali nyingi zilizosababishwa na watu wa bodaboda. Watu wasiostahili kupoteza maisha yao wameyapoteza kwa sababu ya waendeshaji wa bodaboda kutokuwa na umakini. Hili ni jambo sugu katika nchi yetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}