GET /api/v0.1/hansard/entries/1561789/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1561789,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561789/?format=api",
"text_counter": 577,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
"speaker": null,
"content": "Katika mahospitali ya Kaunti za Kilifi na Malindi, kuna wadi zinazoitwa Bajaj Wards. Watu wanaopatikana katika wadi hizo ni wale waliopata ajali kupitia bodaboda. Kwa hivyo, bali na kuwa wamefanya kazi nzuri, wachache wasio na umakini wamesababisha hasara kubwa sana. Itabidi watu hospitalini wafanyiwe operesheni na kuwekewa vyuma. Wakati mwingi utapata hawana pesa za matibabu na inatubidi sisi kama wanasiasa tufanye michango ili wasaidike."
}