GET /api/v0.1/hansard/entries/1562144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1562144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562144/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika. Waziri ana mikakati gani katika sera ya kuongeza zile pesa za ziada kwa wafanyakazi wetu wa umma haswa katika vikosi, kama vile polisi, wanajeshi, walinda misitu na kadhalika? Kwa sababu mbali na kuwa wanafanya kazi katika sehemu ngumu, na sehemu kame, wanafanya kazi katika sehemu ambazo usalama wao pia uko hatarini. Je, ni mikakati gani tutawapatia hao wanaolinda taifa letu; wanaojitolea mhanga katika kulinda Taifa la Kenya? Ahsante, Mhe. Spika."
}