GET /api/v0.1/hansard/entries/1562148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562148/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, UDM",
"speaker_title": "Hon. Chiforomodo Mangale",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Kwanza nataka niseme kwamba eneo Bunge la Lungalunga lina vigezo vyote ambavyo Waziri amevitamka ili kwamba walimu na wafanyikazi wapate hizi pesa za ziada. Maeneo kama Mkwiro na Wasini ni visiwa ambavyo wafanyakazi wanahitajika kuvuka maji ya bahari kila siku kuenda kufanya kazi visiwani Mkwiro na Wasini na kurudi jioni. Maeneo yale ya Mwereni, Dzombo na kule Lungalunga yana shida ya maji na makaazi ya wafanyakazi hakuna. Ile Multi-Agency Team ilienda ikafanya kazi yake, ikamaliza na ikaleta ripoti kwa ofisi hizi za Serikali. Sasa nataka niulize Mhe. Waziri Mkuu—kama hilo jina linastahili—ni lini watu wa Lungalunga, walimu na wafanyakazi watapata haki yao? Hii ni kwa sababu maeneo kama Kinango yanapata faida ilhali vigezo ni hivyohivyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}