GET /api/v0.1/hansard/entries/1562323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562323/?format=api",
"text_counter": 499,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika. Ningependa kumpongeza Waziri. Ningependa pia kumwambia kuwa sheria zikitengenezwa, ahakikishe zinafikia sehemu zote. Kule kwangu, hakuna barabara iliyojengwa kwa sababu contractor hawezi kufanya barabara moja pekee. Hii ni kwa sababu gharama ya kubeba material na meli ni milioni nne. Kwa hivyo, lazima contractors washikane ili waweze kujenga barabara. Hii ni sheria iliyowekwa bila kuzingatia hali yetu. Barabara mbili zilizotengwa bado hazijatengenezwa. Kule kwetu, watu wanangoja lami na ngoma. Tunasikia kuwa barabara ya kwanza ya lami itajengwa. Hatuna hata one-inch ya lami, lakini sasa tunatarajia watajenga. Tunaomba wafanye bidii ili contractor aje. Watu wanangoja sana kwa sababu itakuwa barabara ya kwanza ya lami. Tuko na hamu ya kungoja contractor. Kila wakati watu wanauliza contractor atakuja lini. Tunaomba aje haraka ili nasi tuone lami kwenye barabara hii moja ili tusiwapeleke wanafunzi sehemu zingine kuangalia lami."
}