GET /api/v0.1/hansard/entries/1562609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1562609,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562609/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante sana kwa nafasi hii. Nawapa kongole Maseneta ambao wamemfokea Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi ambaye ameanza kuonyesha utovu wa nidhamu. Mamlaka imemwingia kichwani. Amekosa kuheshimu Seneti kama Bunge la kuwakilisha raia. Najihusisha na matamshi ya mheshimiwa Mungatana. Kenya hii ina kaunti 47, zaidi ya maeneo bunge 290 na wadi zaidi ya 1000. Makabila yote yamo hapa nchini. Iwapo mawaziri watakuwa wanazingatia maeneo yao na kutenga fedha za kuwatetea makwao, hakuna haja wao kuleta stakabadhi za kupitishwa hapa Seneti. Waende katika vijiji vyao kupitisha bajeti zao. Watuachie sisi Bunge la Seneti na la Kitaifa kuwatetea Wakenya. Bw. Spika, ni dhahiri shahiri kwamba hali sio nzuri hapa Kenya. Kila mara sisi ambao tuko mrengo wa serikali tunawatetea kutunga sheria. Tunaketi hadi usiku wa manane kuhakikisha kwamba sheria tunazotunga zinaboresha maisha ya wananchi. Hatuwezi kesha hivyo kisha yule tuliyempa mamlaka na nafasi ya kuamrisha jinsi fedha zitatumwa, anatupiga teke. Hatubembelezani hivyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}