GET /api/v0.1/hansard/entries/1562612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562612,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562612/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Nazungumza kwa niaba ya watu wa Bungoma. Wametangaza kwamba wanapandisha hadhi ya hospitali ya Bungoma. Ni sawa, tumekubali. Ila iwaje mtu atangaze fedha za kuenda kwao ilhali sisi tunaambiwa wamepandisha? Kupandisha nini? Katika nyumba zao, ukiamka kuna vitu unapandisha. Katika serikali, bendera hupandishwa. Kwa hivyo, ni lazima watueleze wamepandisha nini katika kaunti hizi zote ili Mkenya afurahi kwamba tunaunga serikali mkono. Hatutakubali upumbavu, kiburi na fedheha tunayoona. Naomba kama Jumba la Seneta, amurishwe kuja hapa. Huko kwetu akija akibwatabwata kitaumana. Sisi sio watoto. Sisi ni viongozi tuliopigiwa kura. Tunawaheshimu, wao pia watuheshimu. Njia ni mbili. Asante sana."
}