GET /api/v0.1/hansard/entries/1562920/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562920,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562920/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kujiunga na wenzangu kumuomboleza marehemu Mbunge wa Kasipul Kabondo, Ong’ondo Were. Ninatoa rambirambi zangu kwa familia, marafiki na wakaazi wa sehemu hiyo kwa kumpoteza Mbunge wao kwa njia tatanishi. Bw. Spika, ikumbukwe kuwa Mbunge huyo alikuwa ametoa malalamishi katika vitengo vya usalama. Hata hivyo, malalamishi hayo hayakuchunguzwa na matokeo yake ni kuwa Mbunge wetu amefariki. Kweli dunia ni jukwaa. Amefariki kwa njia ambayo inatukumbusha sisi kama Wabunge kuwa masuala ya usalama siyo tu ya Mbunge bali kwa kila mtu pale nje. Inasikitisha kuwa kama Mbunge anayewakilisha idadi kubwa ya wananchi anaweza kuuawa kwa njia hio, sembuse raia wa kawaida? Bw. Spika, ningependa kujiunga na wenzangu ambao wanasema jambo hili lichunguzwe ili tuweze kujua mauaji haya yalitekelezwa na nani na nia ilikuwa ipi, ili tusipoteze maisha katika njia kama hio. Nikisoma katika vyombo vya habari, naona kuwa kuna askari wanaohusika katika mambo kama haya. Najua siyo askari wote wabaya ambao wanatekeleza mambo kama hayo. Kwa wale wote wabaya ambao wanatekeleza mambo kama hayo, wajue kuwa dunia ni jukwaa, leo ni wewe, kesho mwingine. Mungu ailaze roho ya marehemu Mhe. Charles Ong’ondo Were pahali pema peponi. Asante sana, Bw. Spika."
}