GET /api/v0.1/hansard/entries/1562921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562921,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562921/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza ninataka kutoa rambirambi zangu kwa familia, jamii, marafiki na wale wote waliokuwa karibu na familia ya Mhe. Charles Ong’ondo Were. Kama tunavyoelewa ni kwamba hivi sasa familia wanalia kwa sababu wamempoteza mzee wao. Familia ya Mhe. Were iko katika huzuni wakati huu. Sio kwamba wakati wa Mwenyezi Mungu kwake wa kufa ulikuwa umefika lakini ni mambo ambayo yaliyotendwa na majambazi. Jambo la kusikitisha kabisa ni kwamba baadhi ya hao majambazi wengine wao ni polisi. Hili ni jambo la kusikitisha sana ikiwa sisi sote tunalindwa na askari halafu hao askari wanatuendea kinyume."
}