GET /api/v0.1/hansard/entries/1562923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562923/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tunataka uchunguzi ufanywe kisawa sawa. Wale watakaopatikana na hatia, hukumu iweze kupeanwa vile vile kisawa sawa, kwa sababu jambo waliotenda ni la kusikitisha. Bw. Spika, wakati huu waheshimiwa wengi wako katika hali ya sintofahamu ya kuogopa; kutojua ni nani mwingine ambaye ataangushwa na risasi. Kutokana na hicho kitendo kilichofanyika kwa mheshimiwa, tunaomba waheshimiwa wengine wajue ya kwamba kama uko na askari na hawezi kukutetea, ikakuwa ni jambo la kusikitisha. Kwa wale ambao wamefiwa na mpendwa wao, ninaomba tuwaweke mbele ya Mwenyezi Mungu, tuwaombee na tujue ya kwamba hilo ni kosa ambalo lilifanyika. Ni mauti ya Mhe. Ong’ondo Were ambayo ilifanyika na kwamba Mwenyezi Mungu ataiweka roho yake mahali pema peponi. Asante, Bw. Spika."
}