GET /api/v0.1/hansard/entries/1562955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1562955,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562955/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "kubwa sana. Siku hiyo nilikuwa humu Bungeni kufuata mambo yangu na nikapatana naye hapa chini. Nilikuwa na karatasi yangu ya Bunge Sacco. Aliniambia nimsubiri kidogo, lakini nilikimbilia mtu mwingine aliyenitilia sahihi. Baadaye jioni, nilipata habari kwamba alikuwa ametuacha. Kuna haja sisi viongozi kupata ulinzi wa kutosha kabisa kwa sababu mlinzi mmoja wakati huu hatoshi. Huyu alipigwa risasi akiwa na mlinzi wake mmoja. Je, sisi wengine tulio na mlinzi mmoja tutakuja kumalizwa wakati mmoja? Naomba Maseneta wenzangu tuhakikishe kwamba tumeongezwa ulinzi wa kutosha. Kama mwenzetu ameondoka, hatujui tutakuwa namna gani kesho. Ninatoa rambirambi zangu kwa familia ya marehemu. Mungu amlaze mahali pema peponi. Sisi viongozi tujihadhari na kujikinga kwa sababu mauti hutokea wakati wowote. Hata hivyo ni lazima tuongee na kusema ukweli kwamba tupate ulinzi wa kutosha. Au sivyo? Mbona hamsemi tuongezewe?"
}