GET /api/v0.1/hansard/entries/1562957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1562957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562957/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kujiunga na Maseneta wenzangu pamoja na wewe kutoa rambirambi zetu kwa mwendazake Mhe. Charles Ong’ondo Were. Mwaka juzi tulitembelea nyumbani kwake tukiwa tumekwenda mkutano kule Homa Bay na akatufariji kwa chakula cha mchana siku hiyo. Tulijua kweli alipendwa na watu wake na hakuwa mtu wa kutaka makubwa. Mara nyingi utampata hapa Bunge akifanya kazi yake bila kufanya mambo isiyo ya kawaida. Kwa hivyo, kifo chake ni pigo kwa chama chetu cha ODM, Bunge na taifa. Ninasema hivi kwa sababu ameuliwa katika hali ambayo inatatanisha. Bw. Spika, usalama umezorota nchini. Kuna haja ya taasisi husika, Waziri, Inspector General wa Polisi na taasisi zingine husika kuchukua hatua ya haraka ili kujaribu kuzuia kuzorota kwa usalama katika nchi yetu ya Kenya."
}