GET /api/v0.1/hansard/entries/1562961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1562961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562961/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa ruhusa ili niweze kutoa rambirambi zangu, ya familia yangu na ya watu wa Embu County. Huyu Mbunge wa Kasipul Kabondo alikuwa rafiki yangu. Ni ajabu kwamba hiyo mambo ilifanyika. Sisi kama waheshimiwa, hatukufurahia hicho kitendo. Naomba familia yake na watu wa eneobunge lake wakae vizuri. Pia ningewasihi waombe ili waendelee kuishi vizuri. Wakati ukifika wa uchaguzi, wachague mtu ambaye atafanya kazi kama Mhe. Were. Inahuzunisha vile gari lake lilifuatwa kutoka hapa Bunge mpaka wakati alipopigwa risasi kwa traffic jam . Tuliona kwa picha vile yule mtu alitoka kwa boda boda na akaenda akamuua. Mambo ya ajabu ni kwamba lile gari lilikuwa na driver na askari, ilhali hicho kitendo kilifanyika. Hebu jiulize kile ambacho wananchi wa kawaida wanaweza fanya. Hakuna vile yule askari angeweza kutoka kwa lile gari na aweze ku- shoot yule mtu? Hiki kifo ni kitu cha kuhuzunisha. Kwa hivyo, tunapaswa kujiangalia. Lazima tuishi vizuri na wale watu ambao tunafanya kazi nao. Ulinzi wetu pia uangaliwe. Tuliona vile Mhe. Rais alitupiwa kiatu kule Migori alipokuwa anahutubia wananchi. Ni lazima"
}