GET /api/v0.1/hansard/entries/1562968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1562968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1562968/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13733,
        "legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
        "slug": "agnes-kavindu-muthama"
    },
    "content": "Kenya imepoteza. Hii ni kwa sababu hakukuwa akitetea watu wa eneo bunge lake peke bali alikuwa akitetea watu wote wa Kenya. Kwa hivyo, Wakenya wanafaa kulia kwa jumla. Ningependa kurudia kile ambacho Sen. Beth Syengo amesema. Hata mwizi akikufa, tunafaa kujua ya kwamba yuko na wazazi, watoto na watu ambao wanaomboleza. Hao watu huwa na majonzi kwa sababu hawakujua uovu wake. Kwa hivyo, Wakenya wangeshikana pamoja. Kama kuna watu ambao wana sababu zingine zaidi ya hizo, wafuate njia zinazostahili. Sio vyema kuweka mzigo mwingine mzito kwa familia wanapoendelea kuomboleza. Kama taifa, tuko na jukumu la kuajibika. Ninataka kusema hii kwa sababu imenihuzunisha. Wakati Mhe Rais wa Kenya alipokuwa akiongea, kiatu kilirushwa kikamgonga mkono. Bw. Spika, niko upande wa upinzani lakini siwezi kufurahia kitendo kile. Raisi ni kiongozi na kama mzazi. Je, mtoto akichukua kiatu na kumrushia mzazi, itakuwaje? Hata kama tunalia kwamba kuna mambo hayaendi inavyostahili, lakini kuna pahali hatufai kufika kama taifa. Kama taifa, tuko na jukumu la kuwajibika. Ningeomba kitendo kama hicho kisitendeke tena. Natoa rambirambi zangu kwa watu wa Kaunti ya Homa Bay na Machakos. Asante."
}