GET /api/v0.1/hansard/entries/1563139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1563139,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563139/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kwanza, ninapongeza Kamati hii pamoja na ile ya Bunge la Kitaifa kwa kumaliza zoezi hili la kuwapiga msasa wale wateule wanne wa nyadhifa hizo. Mhe. Spika, inasikitisha kwamba ijapo kuwa uteuzi wa wakurugenzi wa bodi ni muhimu sana, jukumu la Bunge ni ndogo sana. Jukumu la Bunge ni kupitisha yale majina yaliyofanyiwa uchunguzi na taasisi zingine. Hata kama Bunge lingependekeza kwamba kuna mtu aliyeteuliwa ambaye hafai katika nyadhifa fulani, halikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kuna haja ya kurekebisha sheria ili pia sisi tuwe na uwezo wa kukataa wale wanaoteuliwa. Kuna wengine hawafai kuwa katika wadhifa huo, lakini kwa sababu mikono yetu imefungwa, hatuwezi kutoa mapendekezo yoyote kuhusu wale walioteuliwa na majina yao kuwasilishwa Bungeni."
}