GET /api/v0.1/hansard/entries/1563141/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1563141,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563141/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Katika uteuzi ule, yule kijana wa mwisho alinifurahisha na maelezo yake ya mambo aliyoweza kuyafanya kwa ule muda ameweza kuhudumu katika nyadhifa tofauti katika nchi za kigeni pia. Amependekeza mambo muhimu kuhusu masuala ya fedha. Sasa hivi, kuna suala ibuka la crypto currency. Masuala kama haya ni muhimu na inafaa wakurugenzi wa Benki Kuu ya Kenya wawe na ufahamu na uwezo wa kuyafafanua na kutoa mwongozo kwa taifa kuyahusu. Kuweka mtu yoyote anayetafuta kazi kama tunavyoona kwa tume nyingine inapelekekea kulemaa kwa tume nyingi. Kwa mfano, Kenya National Human Rights Commission na National Gender Equality Commission zimelemaa kwa sababu ya kuweka makamishina ambao hawajui kazi zao vizuri. Nimefurahi kwamba kumepata mwanachama wa bodi ya kitaifa. Tunatarajia kwamba wale wengine watakaochaguliwa kwa siku za usoni watakuwa ni watu wenye tajriba ya kuwezesha kusaidia bodi hizi na kusaidia nchi kuweka misingi thabiti ya masuala ya fedha katika nchi yetu. Asante kwa kunipa fursa hii."
}