GET /api/v0.1/hansard/entries/1563687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1563687,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563687/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Taarifa yaliyoletwa Bungeni na Sen. Hamida. Ni kweli kwamba baadhi ya mashirika ya ndege yanayohudumu katika nchi yetu, hususan Turkish Airlines na mengineyo, huduma za viwango vya juu wanazotoa yanaacha maswali mengi kuulizwa kuliko majibu. Nilibahatika kusafiri kwa ndege ya Turkish Airlines kuenda Istanbul hivi majuzi. Huduma za Business Class kwa ndege ile ni tofauti za zile zinazotolewa kwa kiwango hicho hicho kwa ndege zinazosafiri kutoka Istanbul kuenda maeneo mengine kama Europe, America na Asia. Haiwezekani ndege ile ile itoe huduma tofauti kwa watu wanaokuja Africa na wale wanaoenda sehemu ingine. Sijui shirika linalothibiti huduma hizi katika nchi yetu ya Kenya linafanya nini ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinafikia viwango vinavyotakikana. Tunaomba Kamati iharakishe kuchunguza suala hili kwa sababu Wakenya wengi wanapata shida. Inaonekana kuna ubaguzi wa rangi katika huduma wanazotoa maeneo ya Africa na maeneo mengine wanayohudumu. Mhe. Spika, naunga mkono maombi ya Taarifa ya Sen. Hamida Kibwana. Asante."
}