GET /api/v0.1/hansard/entries/1563705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1563705,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563705/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Jambo la tatu ni kuwa kuna viwanda ambavyo vimejengwa kule Sagana. Tunaambiwa kuwa tunafaa kwenda huko kutafuta huduma kwa sababu shamba lililoko Mji wa Ngurubani linapakana na maghala ya Halmashauri ya Nafaka, mahali ambapo wakulima wanaenda kuchukua mbolea ya ruzuku. Pahali hapo panaposemekana kuwa katikati ni Zaidi ya kilomita 30. Ni kama kutoa jikoni karibu na sebule na kuipeleka karibu na bafu. Inafaa kuwa mahali ambapo unaweza kutembea."
}