GET /api/v0.1/hansard/entries/1563762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1563762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563762/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Thank you, Madam Temporary Speaker, for giving me this opportunity. Asante kwa kunipa hii fursa niweze kuchangia Hoja hii ya bursary. Kuna mambo mengi ambayo yanahusika na bursary. Ukienda kwa nyumba za waheshimiwa kule mashinani, utapata watu wakiwa huko wakingoja kupewa bursaries. Hali hiyo pia hukua katika nyumba ya Members of County Assemblies (MCAs) na governors. Hoja hii ni nzuri lakini tukitaka kuondoa bursaries, lazima tuanze na ofisi za juu kisha tutoe bursaries kwa maofisi za governors na Members of Parliament. Baadaye, hiyo pesa iwekwe pamoja na kupewa Ministry of Education ndiposa elimu iwe bure kuanzia shule ya chekechea hadi university. Hata pesa inayotumika kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi pia ipewe Ministry of Education ndiposa elimu iwe bure nchini. Hii itawezesha kila mtoto, hata yule maskini, kusoma bila kusumbuliwa. Sisi kama maseneta tunasumbuliwa sana na mambo ya bursary ilhali hatupati hizo pesa. Wananchi hutupigia simu kuitisha karo ya shule. Hiyo pesa ya bursary ikiwekwa kwenye kikapu kimoja na masomo iwe bure, shule zitaendelea na watoto wote watasoma. Hatutakuwa tukifanyia watoto harambee kwa sababu hawajapewa bursary. Naomba yule mtoa Hoja hii aone vile ataongeza kile ambacho nimesema juu yake Hoja hii. Hiyo ikifanyika, watoto wote watasoma."
}