GET /api/v0.1/hansard/entries/1563763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1563763,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563763/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa muda. Ninaunga mkono Mswada ambao uko mbele yetu. Kuna mambo mengi katika Hoja hii ambayo yanafa kuangaliwa. Tumekuwa tukipitisha pesa ziende kwa national Government na kaunti zetu lakini mipango huwa haifuatiliwi vizuri. Hoja hii inahusu mambo ya elimu lakini lazima iangaliwe kwa njia inayofaa. Kenya ni nchi ya demokrasia na mambo mengi lazima yarudishwe kwa wananchi ili waweze kuamua kile ambacho wanataka. Tumepitisha sheria nyingi ambazo zinaleta shida kwa wananchi, county governments, National Treasury na kona zote za hii nchi. Hili jambo lazima liangaliwe na njia inayofaa ndiposa tuhakikishe ya kwamba elimu itakuwa free kutoka kule chini hadi university. Ikiwa hivyo, mimi nitaiunga Hoja hii mkono. Lakini lazima tufanye public participation kabla tuamue kwa sababu wananchi lazima waseme vile wanavyotaka kuongozwa. Tumeona pesa ikienda kwa NG-CDF na Wabunge wanazitumia kupeana bursary. Kaunti, national Government na MCAs pia wanapeana bursaries ilhali pesa hiyo haitoshi. Inawezekana pia hiyo pesa haifanyi kazi vile inafaa. Tunaweza kuwa tunalaumu viongozi bila kuangalia pahali ambapo pesa inapotea. Inaweza kuwa ya kwamba National Treasury iko na shida. Tukitaka Hoja hii isaidie Mkenya, lazima tufanye audit inavyofaa. Hii pesa ikienda kwa Ministry of Education, mtoto yeyote asiitishwe pesa. Tumeona Ministry of Education wakipewa pesa ilhali kumekuwa na malalamishi. Kumekuwa na vita vingi katika primary na secondary schools. Shule zingine huwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}