GET /api/v0.1/hansard/entries/1563764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1563764,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1563764/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "zinafungwa mapema ama watoto hawapewi chakula ilhali mwalimu mkuu hawezi rudisha watoto nyumbani kwa sababu ya karo. Audit nchini Kenya haifanywi vile inafaa. Hiyo inafaa iangaliwe. Kaunti zingine zina shida kwa sababu ya jua kali na ukosefu wa maji. Mfano mzuri ni Mbeere North na Mbeere South katika Kaunti ya Embu. Hizi ni sehemu kavu. Walimu huwa hawana maji ya kuoga, stima na hata hakuna hospitali. Hao walimu husafiri kama kilomita 30 ilhali inasemekana ya kwamba hawatapata hardship allowance. Ninaomba ya kwamba hiyo ikome ndiposa hardship allowance iendele katika kaunti kama Embu. Wakitoa hiyo allowance, itakua vigumu mwalimu awezekusaidia mtoto asome kutoka nursery, primary mpaka aende secondary school. Walimu ambao wako Embu ya juu hawapati ile pesa na wanaumia. Uzuri ni kwamba hao wako na maji na barabara ya lami sio kama walimu ambao wanafundisha Mbeere North na Mbeere South. Hii shida haipatikani Embu County peke yake. Ninaomba hiyo mambo ya hela iangaliwe. Naomba watu ambao wanaleta Hoja katika Parliament wahakikishe ya kwamba imefanyiwa upelelezi ndiposa isilete mgawanyiko nchini Kenya. Sisi sote tunajua ya kwamba nchi yetu ambayo inaongozwa na Mhe. Rais Ruto inapenda amani na tunataka muungano ndiposa kaunti zote 47 ziendele mbele. Mambo ya pesa lazima irejeshwe kwa wananchi ili wasema katika public participation vile wanataka wapewe pesa. Tunaweza sema pesa ipelekwe kwa ministry kisha hiyo ministry ikose kufanya kazi. Naunga mkono free education. Ni lazima masomo shule zote iwe free nchini. Huwa tunasema ya kwamba kaunti zipewe pesa na National Treasury inakataa kupeana pesa. Walimu wanateseka wanapo retire kwa sababu wanapata ya kwamba hakuna pesa. Lazima mambo ya elimu iangaliwe kikamilifu kabla tuipitishe Hoja hii. Kwa hivyo, mimi siungi mkono Hoja hii."
}