GET /api/v0.1/hansard/entries/1564017/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1564017,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564017/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ninachukua fursa hii kuongeza kauli yangu kwa hii taarifa iliyoletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu kuhusu uteuzi wa makamishna wa IEBC. IEBC ni kiungo muhimu cha uchaguzi katika nchi yetu ya Kenya na makamishna hawa pamoja na mwenyekiti wao watakapofanya kazi, itakuwa ya kuangalia uchaguzi wa Rais, magavana, maseneta, wabunge wa Bunge la Taifa na vile vile wabunge wa kaunti. Uteuzi wao lazima upitie katika Bunge la Seneti kwa sababu Seneti ina linda masilahi ya ugatuzi; bunge za kaunti na masilahi ya magavana. Haiwezekani kwamba sheria inayotumika kuwachagua ni ile ambayo iliyofanywa kabla ya kuwa na mfumo wa ugatuzi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}