GET /api/v0.1/hansard/entries/1564031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1564031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564031/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuongea kuhusu Taarifa inayohusu usalama katika basi na usalama wa abiria. Watoto wetu haswa wakati wa kufunga na kufungua shule huwa wanasafiri sana kwa barabara zetu. Ni lazima sasa kamati inayohusika waangalie kama itawezekana hizi SACCO ambazo zinafanya kazi kwa upande wa matatu na mabasi ziongezewe masharti kwamba wanapoondoka Nairobi kwenda Mombasa na kwingineko, wawe wanatoa cheti kuonyesha kwamba wamefanya ukaguzi kwa wanaoabiri magari hayo ili kuhakikisha kwamba wako katika hali ya usalama. Mara nyingi, katika usafiri, watu wanaangalia pesa, bima, viti vimekaliwa au havikukaliwa. Pia, kuna ajali ama hakuna; madereva wamelipwa au la. Usalama wa abiria haungaliwi. Ningependa sana wakati Kamati hii inapoangalia suala hili lote iangalie pia na usalama wa abiria."
}