GET /api/v0.1/hansard/entries/1564386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1564386,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564386/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mhe. Spika, pia mimi najiunga na Maseneta waliotangulia kuchangia Hoja hii kwamba yanayoendelea katika Kaunti ya Nyamira ni makosa. Hoja hii ilipokuja kwa mara ya kwanza, kabla ya Kamati kuambiwa ichunguze, suala hili lilikuja katika hali isiyokupendeza. Kuna bunge mbili katika Kaunti ya Nyamira yanayotoa mwongozo tofauti kwa serikali ya Kaunti ya Nyamira. Ni lazima Gavana wa Kaunti ya Nyamira alaumiwe kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa mambo yote. Ijapokuwa Bunge la Kaunti lina nafasi ya kufanya maamuzi yake kibinafsi, masuala yote yanapitia katika meza yake. Ni aibu kwamba hata baada ya Kamati kwenda, mabunge yale mawili hayakuweza kuamua ni Bunge lipi halali. Tukiacha suala hili liendelee, litaenea katika Mabunge mengine. Vilevile, itakuwa shida kutatua. Kila mtu ataona kwamba ana haki ya kutoa Kenya Gazzete kwamba watakuwa na kikao mahali fulani huku wananchi wanapata shida na pesa za umma zinaendelea kufujwa. Kuna haja ya suala hili kutatuliwa kwa haraka. Ikiwa korti imesema hakuna amri ya kuzuia kubanduliwa kwa Spika aliyebanduliwa, ilhali yule spika mwengine ameshaapishwa, hakuna sababu ya kuwa na mabunge mawili. Tusubiri mahakama itakapoamua kesi hiyo. Tukiachana na suala hili, kuna siku tutasikia kuna Naibu Rais amefungua ofisi mahali fulani na anafanya kazi kwa wananchi wa Kenya akiwa na Wabunge wake. Asante, Mhe. Spika."
}