GET /api/v0.1/hansard/entries/1564435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1564435,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564435/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mumma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Sen. Kinyua, kwa kukubali nikujulishe. Ningependa kufahamisha Seneti kwamba hili suala halikuangaziwa na Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali pekee. Spika aliamuru kuwa Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu iangalie mambo ya kisheria yanayohusiana na mambo ya Nyamira. Kile ambacho hatujaelezwa leo ni ikiwa Kamati hiyo ilimaliza ripoti hiyo au kama ilitekeleza majukumu iliyopewa na Spika. Si vizuri kuendelea kukashifu Kamati moja ilhali hatujapata ripoti ya kamati ya pili."
}