GET /api/v0.1/hansard/entries/1564446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1564446,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564446/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "kushughulika jambo hilo ilhali katika Kaunti ya Nyamira, pesa zinaendelea kutumika kwa njia isiyofaa kwa sababu wanaendesha vikao viwili. Kamati hiyo inayoongozwa na Sen. Wakili Sigei haioni kama hilo ni jambo ambalo linafaa kushughulikiwa kwa dharura. Wanapaswa kuleta ripoti kama ilivyofanya Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali. Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu haijafanya chochote ilhali wao ndio wanapaswa kushughulikia jambo hilo. Kwa kumalizia, naona Gazette Notice ya tarehe 23/11/2024 ambayo inasema kwamba wamekubali kuwe na vikao Masaba North Sub-County Office, Nyamira Sub- County Office, Manga Sub-County Office, na Borabu Sub-County Office. Swali langu ni, je, kwa nini Idara za Serikali zinakubali mambo kama haya kutendeka? Bw. Spika wa Muda, naunga mkono kwamba vikao hivyo visitishwe. Wanafaa kuwa na kikao kimoja ambacho kinakubalika. Nashukuru."
}