GET /api/v0.1/hansard/entries/1564552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1564552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564552/?format=api",
    "text_counter": 379,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Ningependa kushukuru Sen. Omogeni kwa kuleta Taarifa hii ambapo aliuliza maswali matatu. Kwanza, alitaka kujua ni kikao gani kinachofaa kuketi katika Bunge la Kaunti ya Nyamira ambalo liko katika Taarifa ya Gazeti la Serikali. Pili, alitaka kujua uhalali wa sheria ambazo zinapitishwa na mabunge yote mawili, ikiwemo bajeti ya ziada. Tatu, aliuliza Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali njia ambazo zilitumika kuchagua Spika na Katibu wapya."
}