GET /api/v0.1/hansard/entries/1564558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1564558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564558/?format=api",
"text_counter": 385,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Sen. Omogeni alitaja mambo ya Taita-Taveta. Ni kweli kuwa kuna shida katika bunge hilo ingawaje siyo kama Bunge la Kaunti ya Nyamira kwa sababu kule Taita- Taveta, Spika alibanduliwa kupitia kwa impeachment kisha akaenda kortini. Alipoenda kortini, saa hii aliyekuwa Naibu wa Spika ni Acting Spika. Tunafaa tuangalie sheria ili kukiwa na kesi katika korti itachukua muda gani ili yule ambaye ni Naibu wa Spika awache kuwa Acting Speaker? Ikiwa kesi itachukua muda sana kama hii ya Nyamira County, huo mkanganyiko unachukua muda mrefu na katika sheria hakuna Acting Speaker . Kuna Spika na wakati Spika ametolewa lazima kuchaguliwe Spika. Kwa hivyo, hii Kamati pia inaweza ingilia mambo ya Kaunti ya Taita Taveta kuona uhalisi wa mambo ambayo yanaendelea huko. Naunga mkono moja kwa moja ya kwamba, Tume ya maadili la kupigana na ufisadi iingilie ili mambo yanayotokea Kaunti ya Nyamira, yakiwemo kutolewa pesa na CoB kwenda kwa bunge na pia Waziri wa Serikali ya Kaunti ya Nyamira kupeana Form C na kujaza ili bunge hilo lipewe pesa."
}