GET /api/v0.1/hansard/entries/1564719/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1564719,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1564719/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraji",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kumkaribisha Waziri na nimpongeze kwa kufika kwa wakati. Swali langu kwake ni kwamba kuna jinamizi jipya limechipuka katika Taifa letu ya Kenya; jinamizi la watoto wetu kucheza kamari. Kuna ushahidi ya kwamba pesa nyingi zinazochukuliwa katika mifuko hii ya hazina za fedha inaenda kutumika katika hali isiyo ya malengo ya hazina hizi. Je, kuna mikakati gani katika Wizara yetu kuhakikisha ya kwamba tunafuatilia utekelezaji wa ruaza za hazina hizi za pesa? Kuna mikakati gani ya kuhakikisha kwamba pesa zinazochukuliwa zinafanyiwa biashara na zinastawisha vipi uchumi wa serikali kama ilivyokuwa malengo ya Rais wetu wakati alipokuwa anaweka hazina hii ya fedha? Je, kuna sera ya kuona kwamba anayechukua pesa hizi anaenda kufanyia yale malengo yake ama anaenda kutumia kwa mihadarati na hata kujiingiza katika jinamizi la Kamari? Asante, Bw. Spika."
}